PICHA: Lowassa Alivyoshiriki katika ibada ya mazishi ya Mtoto wa Mwakasege

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA Mh. Edward Lowassa ameshiriki katika ibada ya mazishi ya kijana Joshua Mwakasege ambae ni mtoto wa mwalimu wa neno la Mungu Christopher Mwakasege.

Ibada hiyo imefanyika katika kanisa la KKKT usharika wa Mbezi Beach, Dar es salaam mchana wa leo.

Joshua alifariki dunia Octoba 11, 2018 katika Hospitali ya Agha Khan baada ya kuugua ghafla wakati akiwa kazini.

Mwili wa Joshua ambaye ni mtoto pekee wa kiume mwalimu Mwakasege, utasafirishwa kuelekea Tukuyu mkoani Mbeya kwa maziko.




from MPEKUZI

Comments