Lowassa Afunguka na Kutoa Ushauri Mzito Kwa Timu Yetu ya Taifa Stars

Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa amewataka wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kucheza kama morani wa kimasai katika mechi yao ya  leo Jumanne October 16  dhidi ya Cape Verd uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
 
Katika Taarifa yake kwa vyombo vya habari Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa kamati Kuu ya CHADEMA, amewataka wachezaji hao wa Stars kucharuka na kutokuwa legelege uwanjani ili kulipambania Taifa lao.
 
“Kule kwetu masaini tuna vijana shupavu wanaitwa Morani..morani wale wanaua Simba na ni wakali kweli kweli sasa hawa wachezaji wetu wageuke kuwa Morani pale uwanjani..kipigo walichokipata kule kwao(Cape Verde) iwe kama Simba amevamia zizi letu la ng’ombe..wamtoe na kumuua hapana kuwa legelege” Amesema  Lowassa.
 
Aidha Lowassa amelitaka shirikisho la soka nchini TFF kuweka kiingilio cha chini;

 “Nasikia wameweka kiingilio cha shilingi 2000 kule kwa kawaida..mimi ningependa iwe 1000 ili watu waujaze uwanja ule kuwapa moyo Morani wetu”


from MPEKUZI

Comments