Hans Poppe Asomewa Mashitaka Mawili na Kuachiwa Kwa Dhamana

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba, Zakaria Hanspope leo Jumanne October 16 alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka mawili ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo.

Hanspoppe  ni mmoja wa washtakiwa katika kesi inayowakabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake Godfrey Nyange, ambaye alikuwa akitafutwa na Mahakama.

Hanspope alipandishwa kizimbani leo  na kuunganishwa na washtakiwa wenzake wawili, Aveva na Nyange, na kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Kutokana na kuunganishwa katika kesi hiyo, upande wa mashtaka umelazimika kuwasomea mashtaka upya washtakiwa wote watatu.

Kati ya mashtka 10 yanayowakabili washtakiwa wote wanne katika kesi hiyo akiwemo mfanyabiashara Frankly Lauwo ambaye bado hajafikishwa mahakamani hapo, Hanspope anakabiliwa namshtaka mawili tu.

Akimsomea mashtaka hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, kuwa Hanspope anakabiliwa na mashtaka mawili kati ya kumi yanayowakabili vigogo hao wa Klabu ya Simba.

Mashtaka hayo ni pamoja na shtaka la kughushi na kuwasilisha nyaraka za uwongo.

Katika shtaka la kwanza, inadaiwa Aveva na Kaburu wanadaiwa kula njama na kutenda kosa ya matumizi mabaya ya Ofisi na tukio hilo wanadaiwa kulitenda Mei 30, 2016, jiji Dar kwa nia ya kughushi walighushi hati ya malipo ya Mei 28, 2016 kuonesha kuwa Klabu ya Simba ilinunua nyasi bandia za thamani ya Dola za Marekani 40,577, wakati wakijua kuwa si kweli.

Katika shtaka la pili ambalo ni matumizi mabaya ya Ofisi kwa kuandaa nyaraka ya kuomba kuhamisha fedha linalomhusisha Hanspope,

Pia, wakili Kimaro amesema kuwa katika shtaka la tisa, washtakiwa wote kati ya Machi 10 na Mei 30, 2016, waliwasilisha nyaraka za uwongo kuonesha kuwa Klabu ya Simba ilinunua nyasi bandia kwa thamani ya Dola za Marekani 40,577, wakati wakijua kuwa ni uwongo kinyume cha Sheria ya Kodi ya Mapato.

Hanspope amekana mashtaka na wakili wa Hanspoppe, Augustine Shio alimuombea dhamana mteja wake akidai kuwa mashtaka dhidi yake yanadhaminika.

Hakimu Simba alitaja masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili kutoka Taasisi inayotambulika Kisheria, watakaosaini saini bondi ya Sh 15milioni kila mmoja.

Hanspope ametimiza masharti ya dhamana na ameachiwa huru kwa dhamana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi, Oktoba 19, mwaka huu ambapo washtakiwa hao watasomewa maelezo ya awali(PH).


from MPEKUZI

Comments