BREAKING NEWS : Familia Ya Mo Dewji Yatangaza Dau la Bilioni 1 Kwa Atakayesaidia Kumpata

Familia ya Mfanyabiashara wa Tanzania Mohammed Dewji imetangaza zawadi nono ya TSH. BILIONI MOJA (1,000,000,000)  kwa yeyote atakaetoa taarifa muhimu zitakazofanikisha kupatikana kwa Mfanyabiashara huyo alietekwa.

Dau hilo limetangazwa leo October 15, 2018  na Baba wa ‘Mo’ Gullam Dewji katika  mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za MeTL zilizopo jengo la Golden Jubilee, Posta jijini Dar es Salaam. 

Mzee Gullam Dewji amesema Mwenye taarifa anaweza kuwasiliana na mwanafamilia Murtaza Dewji kwa namba 0755030014, 0717208478 na 0784783228 na findmo@metl.net

Mo Dewji alitekwa na watu wasiojulikana  Alfajiri ya Alhamisi Oktoba 11, 2018 katika Hoteli ya Collosseum jijini Dar es Salaam alipokuwa amekwenda kwa lengo la kufanya mazoezi.


from MPEKUZI

Comments