Amber Lulu Awatolea Povu Zito Wanaodai Ana Sura Mbaya!

Amber Lulu ameamua kuwatolewa uvivu wale wote wanaomsema vibaya kuhusiana na muonekano wake.

Muimbaji huyo ameeleza kuwa ingawa anasemwa kuwa ana muonekano mbaya ila akijiremba basi anapendeza. Kupitia ukurasa wake Instagram ameandika;

"Raha kujivunia ulicho nacho ???? sura langu bayaa lakin make up inakaa nalipenda sura langu unanita sura mbaya wakati me ndo Mamakoo.
 
"Rafiki mzuri ni yule anaye kuface private na kukwambia ukweli pasipo kutaka sifa or kusema pembeni kama kweli anania ya kukushauli au kukuelewesha lakini life goes on tunashaish nao." ameeeleza  Amber Lulu.

Kwa sasa Amber Lulu ambaye alijizolea umaarufu mkubwa alipokuwa video vixen, anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Vuruga.from MPEKUZI

Comments