Steve Nyerere Ajitosa Sakata la Soudy Brown, Maua Sama....Ataka Waachiwe, Wapewe Nafasi ya Kuomba Radhi

Wakati msanii wa muziki, Maua Sama pamoja na mtangazaji wa kipindi cha Shilawadu, Soudy Brown wakiendelea kusota rumande huku wasanii wengi wakionekana kuwa kimya, muigizaji Steve Nyerere ameibuka na kuamua kulizungumzia sakata hilo.

Steve ameomba wadau hao wa sanaa kuachiwa halafu waje kuomba msamaha kwa wananchi kwa kosa ambalo wamelitenda.

==>>Tazama alichokiandika hapo chini

"Morning .Yapita siku 5 Leo rafiki zetu wapo ndani ,Kwanza kabisa nichukue nafasi hii kuwapa pole sana tena sana,Hili jambo kila kila Mmoja wetu amekuwa analiongelea anavyo JUA yeye wangine kisiasa na wangine wanalisema kama jambo jepesi hivi,MSANII NI KIOO CHA JAMII ,jambo lolote analo fanya basi linaweza kuwa na FAIDA kwa TAIFA letu ama hasara kwa TAIFA letu,.

"Sidhani kama MTU mwenye akiri kabisa kabisa akasimama na KUSEMA kukanyaga NOTI ya TAIFA lako na kumwaga mihela chini ni JAMBO zuri kama yupo huyo MTU huyo basi atakuwa na mapungufu naye.

"Tumefundishwa kulinda na KUHESHIMU chochote kile chenye Alama ya TAIFA,Sasa Naimani kupitia wenzetu na JAMII nyingine kuna la kujifunza hapa TENA kubwa sana,ILA NAJUA MTOTO akinyea mkono wa kulia huukati .Na mkubwa akikosea huchutama kwa kosa.

"Kwanza kabisa hakuna MTU aliye juu ya sheria maana sheria ni msumeno ,Kwa niaba ya wenzetu hawa tunaomba radhi sana tena sana kwa vyombo vyote husika.Imani yangu bado VIJANA hawa KAZI ya kuelimisha JAMII kupitia vipaji vyao inaitajika sana

"MIMI kama KIJANA mwenzao naomba kuchukua nafasi hii kuwaombea radhi naamini hawata rudia na si wao TU hata kwa sisi wangine,Nitafurahi nikisikia wamepewa dhamana ,Nitafurahi nikiona wapo huru na kuja kuomba radhi kwa WATANZANIA ,ambao hawakufurahishwa na tendo hilo ,Maana wakati wewe unakanyaga pesa kuna MTANZANIA anatafuta pesa kwa matibabu TU, mwingine kwa milo 3 TU ,mwingine kwa Ada ya mwanae shule TU, ILA ameikosa. 

"BASI KWA HILI NAAMINI TUTAKUWA TUMEJIFUNZA KITU. Kwa Niaba ya wenzangu TUNAOMBA RADHI. TUNAOMBA KAMA WENZETU WATAPATA DHAMANA BASI LITAKUWA JAMBO JEMA.

"TUNAIMANI MAOMBI YETU YA DHAMANA KWA WENZETU YATAFANYIWA KAZI.NAIMANI HATA WAO WALIVO FANYA IVO HAWAKUJUA KAMA NI KOSA. TUNAOMBA WAPEWE DHAMANA.


from MPEKUZI

Comments