Marekani,China zaingia kwenye vita ya kibiashara

China imesema italipiza kisasi kwa kutoza ushuru wa dola bilioni sitini kwa bidhaa za kutoka Marekani, baada ya rais Donald Trump kutangaza kiwango cha ushuru wa ziada kwa bidhaa zinazoingia kutoka China.

China ilitangaza hivyo baada ya kutangazwa kuwa ushuru wa ziada kuwa dola bilioni 200.

Mvutano huu ni matokeo ya vita ya kibiashara kati ya nchi hizi mbili zenye uchumi mkubwa.

Wizara ya fedha ya China imesema inalipiza kile alichokiita ajenda ya Marekani ya kutazama upande mmoja na biashara yenye ushindani usio wa usawa.

Rais Trump ametahadharisha kuwa atalipa kisasi ikiwa wakulima, wafugaji na wafanyakazi wa kimarekani watalengwa kwenye maamuzi ya China. Amesema milango iwazi iwapo China itataka kuzungumza.

Trump amesema China imepatiwa fursa nyingi na sasa China inataka kufanya mazungumzo.

'' Tumekuwa na biashara isiyo na uwiano sawa na China, mwaka jana tulipoteza kiasi cha zaidi ya dola bilioni mia tano kwa China, hatuwezi kufanya hivyo''
 

Credit: BBC


from MPEKUZI

Comments