Idriss Sultan Amuombea Msamaha Maua Sama

Mchekeshaji wa filamu na muigizaji wa bongo 'movie' nchini, Idris Sultan amemuombea msamaha mwanamuziki Maua Sama kutokana na yaliyomkuta na kushauri mamlaka husika kutoa elimu kupitia mwanadada huyo kwa madai adhabu aliyoipata hadi sasa inamtosha.

"Binafsi ningependa kumuombea msamaha Maua kwa kuwa lengo sio kuivunjia heshima fedha yetu na Benki Kuu kwa ujumla. 

"Katika harakati za kujitafutia ugali makosa yatafanyika tu ila muhimu ni tukae tukumbuke lengo, na sio kukomoana, au kuonyeshana nani anajua zaidi, kuwekeana mabavu. Bali lengo ni kuelimisha jinsi ya kutunza vyetu wenyewe", ameandika Idriss.

Pamoja na hayo, Idriss ameendelea kwa kusema kuwa "ningependa ku-propose mumtumie Maua kuelimisha wengine kupitia 'influence' yake na adhabu aliyopata mpaka sasa tufanye imetosha. Hakuna aliye juu ya sheria ila tuvae tu uhusika wa lengo".

Msanii Maua Sama ambaye taarifa ya kukamatwa kwake ilitolewa Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es salaam, Lazaro Mambosasa hadi sasa bado anashikiliwa  katika kituo cha kati jijini Dar es salaam ambapo inadaiwa zoezi la uchunguzi linaendelea ili kusudi aweze kupandishwa mahakamani kujua tuhuma zake.

Tokea kukamatwa kwa Maua Sama kumeibuka mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii, ambayo kila mmoja anaongea jambo lake kuhusu  suala hilo bila ya kufahamu sheria zaidi zinasemaje.

Benki kuu ya Tanzania (BoT)  Jumanne Septemba 18, ilitoa  onyo kwa wananchi kuheshimu fedha ya Tanzania kwa kuwa ni moja ya alama ya taifa na kuonya kwamba kudhihaki na kukejeli noti na sarafu ni kosa la jinai.


from MPEKUZI

Comments