Alichokisema Mgombea wa CHADEMA Baada ya Kushindwa Ubunge Jimbo la Ukonga

Aliyekuwa Mgombea Ubunge wa (CHADEMA) jimbo la Ukonga Asia Msangi ametoa kauli yake ya kwanza kuwa alitegemea kushindwa uchaguzi huo.

Asia Msangi ameeleza alipokea taarifa kuwa angeshindwa uchaguzi huo kutoka kwa wapiga kura wake kwa kile alichokidai kuhujumiwa katika baadhi ya vituo vya kura ikiwemo kuzuiliwa kwa mawakala wake huku zoezi la kupiga kura likiwa linaendelea.

“…ulimwengu wote umeona mambo yaliyofanyika Ukonga, kwa sababu hata kabla ya uchaguzi nilipokea taarifa kuwa Asia hutoshinda.., wameamua kumuweka yeye (Waitara) ndio mbunge wacha wamuweke lakini Ukonga wameona anaewafaa ni nani? . wengi walinipigia simu kwamba hawapigi kura kwa sababu mawakala wangu waliwasumbua tangu saa 12 asubuhi.”

Uchaguzi huo ulihusisha wagombea 14 akiwemo Murshidi kabilinga (NRA) aliyepata kura 6, Kimosa Mohamed (UMD) kura 16, Rajabu Rashindi (NLD) kura 16, Mbwana Kibanda (UPDP) kura 17, Ngubi Ramadhani (ADC) kura 17, Kuzenga Faustine (UDP) kura 23, Kiambo Richard (CCK) kura 74, Nelbert Obatia wa NCCR-Mageuzi kura 27, Kisena Lucas (SAU) kura 40, Rehema Nasoro Chama cha Wakulima  91, Salama Masoud  (CUF) kura 405, Asia Msangi wa CHADEMA  kura 8676 na Mwita Waitara wa CCM kura 77795.

Kwa mujibu Msimamizi wa Mkuu wa uchaguzi jimbo hilo lilikuwa na wapiga kura 300,609 lakini waliojitekeza ni wapiga kura 88,270 tu ambao ni sawa na asilimia 29 ya wapiga kura waliojiandikisha.


from MPEKUZI

Comments