Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Amjulia Hali Dkt. Kigwangalla Kitengo Cha Mifupa MOI

Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya tarehe 14, Agosti 2018 amemtembelea na kumjulia hali Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla aliyelazwa katika wodi maalum kitengo cha Taasisi ya mifupa MOI,  hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa Kikwete kumtembelea Dk Kigwangalla ambapo awali alimtembelea Agosti 8,  alipokuwa amelazwa Wodi ya Mwaisela akipatiwa Matibabu ya awali.

Kikwete amemtakia kila lakheri katika kipindi hiki kwa kuuguza majeraha ya mkono na sehemu za mwili ikiwemo mbavu ambazo kwa sasa hali yake inaendelea kuimarika kwa mujibu wa Madaktari wa kitengo hicho cha mifupa MOI.

Awali tokea kufanyiwa operesheni ya mkono ameweza kufanya mazoezi taratibu ikiwemo kutembea mwenyewe katika viunga hivyo vya Muhimbili.

Dkt. Kigwangalla alipata ajali ya gari mnamo Agosti 4, 2018 huko Manyara akiwa katika ziara ya kikazi ambapo katika ajali hiyo iliyokuwa na watu 6, watano walijeruhiwa na mmoja alifariki dunia ambaye alikuwa afisa habari mwandamizi wa Wizara hiyo, Hamza Temba.


from MPEKUZI

Comments