Mwanamke Atiwa Mbaroni Kwa Kumuua Mwanae na Mwingi kwa Kumuwekea Mwiko Sehemu za Siri

Wanawake wawili wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma mbalimbali akiwamo mmoja aliyemuua mtoto wake wa kiume wa miaka 11 kwa kumpiga fimbo kichwani.

Katika tukio jingine mwanamke mwingine anashikiliwa na polisi akituhumiwa kumsokomeza mwiko sehemu za siri mtoto wa dada yake mwenye umri wa miaka sita.

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema hayo leo Agosti 14 wakati akitoa taarifa ya matukio mbalimbali ya mkoani humo kwa waandishi wa habari.

Kamanda Mutafungwa amesema matukio yote yametokea katika wilaya za Gairo na Manispaa ya Morogoro na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani mara moja.


from MPEKUZI

Comments