Kamati Ya Bunge Yaitaka Serikali Kukutana Na Wenye Viwanda

Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imeitaka serikali kukaa na wamiliki wa viwanda nchini na kuhakiki gharama za uzalishaji ambazo zimekuwa zikisababisha bidhaa za wazalishaji wa ndani kushindwa kushindana na zinazoingizwa nchini.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Sadick Murad ametoa kauli hiyo  jana Agosti 13, wakati kamati hiyo ilipotembelea kiwanda cha uzalishaji wa mabati na vifaa vingine Alaf.

Murad amesema gharama za uzalisha zimekuwa kikwazo kwa viwanda vya ndani ambazo vinazalisha bidhaa kwa bei ghali ilihali zinazoingizwa nchini zinauzwa kwa bei rahisi.

“Gharama za uzalisha zikiwa fair na wazalishaji wa ndani kupunguziwa kodi za umeme na tozo nyingine, gharama za uzalishaji zitashuka,” amesema ambaye pia ni Mbunge wa Mvomero (CCM).

Aidha, alitoa wito kwa wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, kuisimamia vema Shirika la Viwango (TBS) na Mamlaka ya Mapato (TRA) ili ziendelee kutoa huduma rafiki kwa wazalishaji wa ndani ambao wamekuwa chachu katika uzalishaji wa ajira na ukuzajia uchumi.

Hata hivyo, Katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Joseph Buchweshaija amesema tayari imeandaa mpango maalumu wa kwa kushirikiana na TBS kuondoa bidhaa hafifu sokoni. Tayari tumeanza kuisafisha suala hilo na ninawaahidi kuendelea kutekeleza yote mliyoagiza,” amesema.

Aidha,  Meneja Mkuu wa kiwanda hicho cha Alaf, Dipti Mohanty aliieleza kamati hiyo kuwa umeme umeendelea kuwa mojawapo ya kikwazo kikubwa katika uzalishaji wa bidhaa zao.


from MPEKUZI

Comments