Gigy Money: Natamani Mwanangu Aige Tabia Zangu na Ntamuunga Mkono

Msanii wa bongo fleva na 'video vixen' nchini, Gigy Money amesema atajisikia furaha na amani endapo mtoto wake wakike aliyempa jina la Mayra,atafata nyayo zake.

Gigy ameiambia Enewz ya EATV kwamba, haiwezi ikatokea mtoto akawa na role model tofauti na mtu ambaye amemzaa.

"Kila mtoto yoyote 'role model' wake ni mama yake mzazi hata iwaje.  Huwezi kusema mwanao atakuwa 'role model' wa mtu mwingine. Hivyo mwanangu atakuwa tu vyovyote atakavyotaka kuwa mimi nitampa ushirikiano. siwezi kumlaumu hata akitaka kuwa kama mimi ila ndio ntazidi kufurahi", amesema Gigy.

Pamoja na hayo, Gigy ameendelea kwa kusema "siwezi kujutia kuzaa halafu kingine ni kwamba kujipanga utajipanga baadae huko wala hupaswi kuwaza kuwa itakuaje nikifanya jambo fulani. Maisha ya siku hizi hayana hiyo kitu, Mungu yupo kila siku anatenda".


from MPEKUZI

Comments