CCM waibuka na ushindi kata ya Bugalama.

Na, magdalena kashindye.. Kahama
Chama cha mapinduzi CCM kimeibuka na ushindi katika uchaguzi wa marudio katika kata ya Bugalama iliyopo katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Mkoani shinyanga.

Kwenye uchaguzi huo uliofanyika Agosti 12 mwaka huu Vyama vitatu vilisimamisha wagombea watatu katika kata hiyo na mgombea wa CCM Izengo Josephath alitangazwa mshindi kwa kura 2137 akiwashinda wapinzani wake Stephano Izengo wa CHADEMA kwa kura 571 huku mgombea wa ACT wazalendo Jilala Seni akipata kura 32.

Uchaguzi huo wa marudio ulifanyika kufuatia aliyekuwa diwani wa CHADEMA Izengo Josephath kuhamia chama cha mapinduzi CCM na chama hicho kilimpa ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho.


from MPEKUZI

Comments