Arusha: Mgombea Udiwani CHADEMA Achomwa Visu

Jeshi la polisi mkoani Arusha limefungua jalada la uchunguzi wa matukio ya vurugu katika uchaguzi kata ya Kaloleni jijini Arusha baada ya watu wawili kuchomwa visu huku mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema akishushiwa kipigo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng'azi amesema Lema ametoa taarifa za kushambuliwa sambamba na mgombea wa chama hicho katika kata hiyo, Boniface Kimario pamoja na wakala wake.

Amesema baada ya taarifa hiyo, majeruhi walipelekwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru wanakoendelea na matibabu.

Katika tukio hilo, Lema anadaiwa kushushiwa kipigo na watu wanaodaiwa kuwa walinzi wa CCM wakimtuhumu kutaka kufanya vurugu eneo la Tangi la Maji.

Mbali na Lema, wakala wa Chadema, Ibrahim Ismail amechomwa visu na kulazwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru.

Katika vurugu hizo, pia inadaiwa mwenyekiti wa CCM kata ya Kaloleni, Iddi Mukuru amejeruhiwa kwa kuchomwa visu.


from MPEKUZI

Comments