Madiwani Watatu CHADEMA Wavuliwa Uanachama

Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Mbeya umependekeza kuvuliwa uanachama kwa madiwani watatu wa chama hicho mkoani humo kutokana na utovu wa nidhamu waliouonyesha.

Madiwani hao na kata zao katika mabano ni Geofrey Kajigili (Sisimba), Newton Mwatuboje (Manga)na Hamphrey Ngalawa (Iwambi).

Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, Obadia Mwaipalu ametangaza uamuzi huo leo Jumamosi  Julai 21, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari na kubainisha kuwa  vikao halali vya chama vilivyoketi mara kadhaa kujadili hatua stahiki dhidi ya madiwani vimefikia uamuzi huo.

Amesema kutokana na utovu wa nidhamu, kukiuka katiba ya Chadema na kukaidi utekelezaji wa maazimio ya uongozi wamepeleka mapendekezo yao kwa uongozi wa chama hicho Kanda ya Nyasa ili  hatua zichukuliwe.


from MPEKUZI

Comments