Serikali Yatangaza Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Tano

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe.Suleiman Jafo,amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano haitakuwa na msamaha kwa wanafunzi wa kidato cha Tano watakaochelewa kuripoti shuleni kwa zaidi ya Siku 14 kuanzia Tarehe ya Mwisho ya kuripoti,nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.

Mhe.Jafo ameyasema hayo leo Ofisini kwake Jijini Dodoma akizungumza na waandishi wa habari wa kutangaza Uchaguzi wa Wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano,Vyuo vya Ufundi na Vyuo vya Elimu ya Kati kwa Mwaka wa 2018.

Muhula wa Kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano Utaanza tarehe 15 Julai 2018 hivyo wanafunzi wote waliopangwa kujiunga wanapswa kuanza kuripoti katika shule zao kuanzia tarehe hiyo iliyotangazwa amesisitiza ‘Jafo

Aidha Mhe.Jafo amesema kuwa jumla ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu ni kutoka shule za Serikali,zisizo za Serikali na waliosoma nje ya nchi baada ya matokeo yao kupata ulinganifu wa Baraza la Mtihani Tanzania (NECTA) Jumla ya shule 354 zikiwemo shule tisa mpya nazo zimepangiwa kupokea wanafunzi.

Jumla ya Wanafunzi 70,904 wakiwemo wasichana 31,884 na wavulana 39,020 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha Tano,Vyuo vya Ufundi na Vyuo vya Elimu Kati kwa mwaka huu ni 92,712 kati ya hao wanafunzi wa shule 92,630 na wa  Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima 82 wakiwemo Wasichana 38,078 (41.1%) na Wavulana 54,634 (58.9%)

Hata hivyo Jafo amesisitiza kuwa Fomu zenye mahitaji ya kujiunga na kidato cha Tano (Joining Instuctions) kwa shule zote kidato cha Tano zinapatikana  kwenye tovuti ya OR-TAMISEMI kupitiaa anuani ya www.tamisemi.go.tz.

Kwa upande wa Wanafunzi waliopangiwa kwenye Vyuo vya Elimy ya Kati wanapaswa kuthibitisha kukubali kujiunga na kozi walizochaguliwa kuanzia tarehe ya leo hadi ifikapo tarehe 8 Agosti,2018.Wanafunzi hao watatakiwa kufanya uthibitisho kuwa wamekubaliwa kozi na Vyuo walivyopangiwa kwa njia ya Mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) www.nacte.go.tz

Pia Mhe.Jafo,amewapongeza Walimu,Wazazi na Walezi wote kwa juhudi walizozifanya katika ufundishaji na kuwezesha wanafunzi kufaulu vizuri na kusisitiza kuwa wote mnatakiwa kuwa na Moyo huo wa kuwasimamia na kufatilia maendeleo ya watoto wenu.

Aidha Amewapongeza pia wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano,Vyuo vya Ufundi na Vya Elimu ya Kati kwa kuwahimiza na kuwasisitiza kuendelea kufanya bidii katika kujifunza ili kuweza kufanikiwa na mafunzo ya Elimu ya Juu baada ya kuhitimu Kidato cha Sita na Vyuo vya Elimu ya Kati.

Pongezi nyingine Jafo amezipeleka kwa Wadau wote wa Elimu kwa maana ya Viongozi na watendaji wa Mikoa na Halmashauri mbalimbali pamoja na wananchi kwa ujumla kwa kushiriki kikamilifu kuimarisha miundombinu ya shule ikiwemo maabara na majengo muhimu yaliyowezesha shule kupokea wanafunzi wa Kidato cha Tano kwa mara ya kwanza.


from MPEKUZI

Comments