Serikali Kuandaa Mazingira Rafiki ya Kufanya Biashara Nchini

Baada ya kushuhudia ushiriki mdogo wa sekta binafsi kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Serikali imeandaa mpango kabambe wa kuboresha mazingira ya biashara ili kuongeza ushiriki wao.

Hayo yamebainishwa leo Juni 14, na Waziri wa Fedha na Mipango, Phillip Mpango alipokuwa akieleza changamoto zilizojitokeza kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo mwaka 2017.

Amesema mwaka jana serikali imeendelea na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ambao tayari umetekelezwa kwa asilimia 10, kuliimarisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) lililonunuliwa ndege moja aina ya Bombardier Q400 na ujenzi wa kiwanda na shamba la miwa Mkulazi.

"Katika kipindi hicho kulikuwa na changamoto ya kuchelewa kwa fedha za mikopo na misaada ya wahisani. Serikali imeandaa mpango kabambe wa kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini ili kuongeza ushiriki wa sekta binafsi." amesema.


from MPEKUZI

Comments