Mikopo Sekta binafsi Imeongezeka kwa Bilioni 75

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema mikopo iliyotolewa kwa sekta binafsi katika kipindi cha mwaka 2017 imeongezeka kwa  Bilioni 75

Mikopo hiyo imeongezeka kutoka Sh16.808 trilioni zilizotolewa 2016 hadi Sh16.883 trilioni 2017.

Akizungumza bungeni  leo Juni 14, 2018 mjini Dodoma wakati akiwasilisha hali ya mwenendo wa uchumi kwa  mwaka 2017, Waziri Mpango amesema kiasi hicho ni sawa na ukuaji wa asilimia 1.7 ikilinganishwa na asilimia 7.2 kwa 2016.

Amesema hatua hiyo ilichagizwa na tahadhari zilizochukuliwa na benki za biashara baada ya kuongezeka kwa mikopo  iliyoshindikana kulipwa pamoja na benki hizo kupendelea zaidi kuwekeza katika dhamana za serikali.

“Katika kukabiliana na hilo, serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania, imeendelea kuchukua hata mbalimbali ili kuongeza mzunguko wa fedha na kuimarisha ukuaji wa mikopo katika sekta binafsi, hatua hizo ni pamoja na kupunguza kiwango cha kisheria cha sehemu ya amana kinachotakiwa kuwekwa BoT na benki za biashara,”amesema Waziri

Hatua nyingine ni kupunguza riba za BoT, kupunguza riba za dhamana ya serikali , serikali kuendelea kulipa malimbikizo ya madeni kwa wakandarasi na watoa huduma wa hapa nchini. 


from MPEKUZI

Comments