Hashim Rungwe Asema Yuko Tayari Kujiunga na Akina Mbowe ili Kuongeza Nguvu

Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe amesema kuwa yupo tayari kuungana na upinzani pale muda utakapofika na kujiridhisha kuwa mipango inatekelezeka.

Rungwe amesema hayo wakati akizungumza na eatv.tv ambapo amefunguka kuwa endapo ataridhishwa na muungano huo wa vyama vya upinzani atajiunga ili kuongeza nguvu.

“Bado sijajua wanatekeleza vipi sera zao lakini pindi nitakapopata muda na kueleweshwa zaidi nitaungana nao kwakuwa muda ni kila kitu”, amesema Rungwe.

Rungwe ameongeza kuwa kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa kunapunguza hamasa kwa wananchi katika masuala mbalimbali kwa kile alichodai kuwa mikutano ya kisiasa imekuwa ikiongeza hamasa kwa wananchi.

Hivi karibuni viongozi hao wa vyama vya upinzani nchini ACT-Wazalendo pamoja na Chama cha Demokarasia na Maendeleo (CHADEMA) walitangaza kuunda umoja utakaokuza na kuhamasisha demokrasia unaokwenda kwa jina la ‘United Democratic Front’ utakaohusisha asasi zingine pia na sio siasa pekee.


from MPEKUZI

Comments