Waziri: Wahitimu Elimu ya Juu ni wengi kuliko ajira

Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, ajira na watu wenye ulemavu Mh. Antony Mavunde amesema kuwa Serikali inatambua kuwa wahitimu wa Elimu ya juu ni wengi kuliko mafasi za ajira.

Waziri Mavunde ametoa kauli hiyo bungeni leo wakati akijibu swali la Hadija Ally Mbunge viti maalum (CCM) lililohoji serikali imepanua fursa kwa kuongeza vyuo vikuu nchini, je ni kiasi gani mfuko wa vijana unaweza kuwanufaisha walengwa ikizingatiwa kuwa tatizo la ajira ni hali halisi inayowakabili vijana.

Mavunde amesema “Nafasi za ajira zinazotengenezwa kwa mwaka zimekuwa ni chache kuliko wingi wa vijana hivyo basi serikali imeanza kuwabadili mitazamo kuwa sio wote wanaoweza kukaa maofisini bali wanaweza kutumia uwezo wao na kujiajiri katika sekta za kilimo na shughuli nyingine halali zinazoweza wapatia kipato”.

Waziri mavunde ameongeza kuwa Mfuko wa Maendeleo ya vijana umeweza kufikia vikundi 397 ambapo zaidi ya Bilioni nne zimekwisha tumika kuwezesha vijana kiuchumi.


from MPEKUZI

Comments