Waziri Kalemani azindua ujenzi miundombinu ya gesi

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema mbio za kutatua kero za wananchi kuhusu matumizi mbalimbali ya nishati ikiwamo ya kupikia sasa zimeanza rasmi.

Dk Medard ambaye pia ni Mbunge wa Chato ametoa kauli hiyo leo, Jumapili Mei 20, 2018, wakati akizindua ujenzi wa miundombinu ya kuunganisha bomba la gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.

Uzinduzi huo ulifanyika Ubungo jijini hapa na unatarajia kukamilika Septemba mwaka huu.

Kadhalika bomba hilo la gesi litawaunganisha wananchi 1,000 wa mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara watakaonufaika na gesi hiyo.

“Leo nazindua, lakini kazi kubwa ni utekelezaji na kuwafikishia miundombinu Watanzania ili wapate manufaa ya matumizi ya rasilimali hii ya gesi,” amesema Dk Kalemani.

Amesema ujenzi wa miundombinu hiyo utagharimu Sh 4bilioni kwa awamu ya kwanza na maeneo yatakayonufaika ni Mikocheni, Ubungo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sinza, Shekilango na Makongo Juu.

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba amesema hivi sasa wanafanya usanifu ili kujua watu wangapi watapata huduma ya gesi kwa upande wa Dar es Salaam.


from MPEKUZI

Comments