Madhara Makubwa Manne ya Kupiga Punyeto

Kujichua kuna madhara makubwa hata kama unaona kunakupa raha. Kujichua kunaweza kukufanya ukawa mtumwa wa tendo hili na ukifikia hatua hii basi ni dhahiri kuwa kumeshaathiri afya yako ya akili kwa kiasi kikubwa.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wanasansi wa masuala ya ngono wa nchini Marekani akiwemo Dr. Michael Reece, (PhD, MPH) umebainisha kwamba iwapo utakuwa unapenda kujichua hautaona kama unapata ladha yoyote ya tendo la ndoa na mwenzi wako, lakini sio kweli kama ladha ya mwenzi wako imebadilika au kupotea, la hasha, ila kujichua kumeshabadili akili yako na mbaya zaidi umeshakuwa mtumwa wa kitendo hiki

Unaweza  kupata magonjwa ya akili kama vile sonona. Na kujikuta unaanza kuwachukia watu wa jinsia ya tofauti na wewe, kwa sababu tayari akili yake umeshaathirika kisaikolojia anajiona kuwa haja yake ya kimapenzi anaweza akaitimiza yeye mwenyewe pasipo ushirikiano na mtu mwingine

Lakini pia, kujichua kunachangia kupoteza uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kikamilifu. Kwa mwanaume kunaweza kumsababishia uume kulegea au kuwahi kufika kileleni, na kwa mwanamke kujichua kunampotezea ile hali ya kuhimili tendo la ndoa (sexual drive).

Pia kama utakuwa mpenzi wa kujichua unakuwa kwenye hatari kubwa ya kupoteza nywele na kupoteza kumbukumbu.


from MPEKUZI

Comments