Serikali: Hakuna tiba ya kisukari Dunia Nzima

Wizara ya Afya imesema duniani kote hakuna dawa iliyogundulika kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa kisukari na kupona.

Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustin Ndugulile amesema matibabu yanayotolewa kwa sasa ni kumpatia mgonjwa kiwango bora cha kuishi na kuhakikisha kiwango chake cha sukari mwilini kinakuwa ndani ya kiwango kinachotakiwa.

Dk Ndugulile ametaja dawa hizo ni sindano za  insulin ambayo mgonjwa hulazimika kuchomwa kila siku kwa maisha yake yote pamoja na vidonge ambavyo humeza kila siku.

Katika swali la msingi Mbunge wa Viti Maalumu(CCM), Christina Ishengoma  amehoji Serikali ina mpango gani wa kufanya tafiti kuhusu dawa za kisukari.

Waziri amesema ugonjwa huo huwapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 35 na kuendelea ingawa watoto na vijana wanaweza kupata ugonjwa huo kwa kutozingatia misingi ya lishe.

Amesema kuna tafiti zinazofanywa duniani kote ili kutafuta dawa itakayoweza kutibu kabisa ugonjwa huu ingawa tafiti hizo hazijazaa matunda.


from MPEKUZI

Comments