Ndalichako Aijibu Ripoti ya CAG

Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako, amesema anaitumia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kama changamoto na chachu ya kuendelea kufanya kazi nzuri.

 Ndalicho ameyasema hayo leo Aprili 17 wakati akijibu hoja za ripoti ya CAG iliyosomwa wiki iliyopita bungeni.

 Wiki iliyopita mawaziri wanane walifanya mkutano na waandishi wa habari wakijibu hoja za ripoti ya CAG.

“Serikali ya awamu ya tano kwenye suala la udhibiti haina utani kila mtu ameona kazi ambayo imefanyika, tunapopata ripoti ya CAG, inatupa chachu ya kuendeleza na kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya tano,” amesema

Amesema kama CAG alivyoshauri, watafanyia kazi mapendekezo ya CAG na pia watawachukulia hatua watendaji wanaotumia vibaya fedha za umma.

Ndalichako alizungumzia hoja ya CAG kuhusu ukusanyaji hafifu wa fedha za mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na akasema, tangu serikali ya awamo ya tano iingie madarakani, kumekuwa na ongezeko la ukusanyaji wa madeni hayo.

“Taarifa ya CAG 2015/16 hadi 2016/17    inaionyesha kuwa makusanyo yameongezeka kutoka Sh28bilioni hadi Sh 116bilioni. Hilo ni ongezeko la asilimia 300. Takwimu hazidanganyi,” amesema

Hata hivyo amesema bado makusanyo hayo hayatoshelezi na ameitaka  Menejimenti ya Bodi ya Mikopo kuhakikisha ukusanyaji wa mikopo unaimarishwa.


from MPEKUZI

Comments