Abdul Nondo Aitaka Tanzania iige Kenya

Mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Tanzania (TSNP), Mahmud Abdul Nondo amefunguka na kuitaka serikali ya Tanzania kuiga serikali ya nchini Kenya ambayo imeweza kutoa taulo za kike kwa wanafunzi wote wa kike waliopo mashuleni.

Abdul Nondo amesema kuwa yeye anaamini kuwa serikali ya Tanzania pia inaweza kufanikisha jambo hilo kwa kuwa wanafunzi wengi wa kike wanakosa kufika mashuleni kipindi ambacho wapo kwenye siku zao na kuathiri masomo yao.

"Bado tunaamimi hata Serikali ya Tanzania, inao uwezo mkubwa saana wa kutoa sanitary pads (taulo) bure kwa wanafunzi wa kike dada zetu, kwani takwimu zinaonesha hedhi huchangia kiasi kikubwa wanafunzi hawa kukosa masomo. Kutokana na gharama za manunuzi hasa kijijini.Hoja hii ilipelekwa bungeni na Mbunge wa viti maalumu Upendo Peneza, ila haikujadiliwa aliambiwa kuwa hakufuata utaratibu"

Abdul Nondo aliendelea kusema atashauriana na viongozi wake wa TSNP kuangalia namna wanavyoweza kufanya ili wabunge ambao wanaguswa na jambo hilo wasichoke kuliwasilisha bungeni.

"Nitashauriana na viongozi wenzangu wa TSNP kuangalia namna tunavyoweza kufanya suala hili kama Agenda kubwa zaidi, na kuendelea kufanya ushawishi kwa wabunge ambao wanaguswa na jambo hili ili wasichoke kuliwasilisha bungeni kwa Mara nyingine. 

"Ili serikali ijumuishe mpango huu wa kutoa pads bure katika Sera yake ya elimu bure. Ili wanafunzi hawa wapate haki yao kikamilifu ya kupata elimu kama Kenya imeweza hata Tanzania, tunaweza fanya hivi pia kwa manufaa ya dada zetu hawa" Abdul Nondo


from MPEKUZI

Comments