Wawili washikiliwa kutokana na kifo cha Mwanafunzi

Jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikilia watuhumiwa wawili kufuatia kifo cha kutatanisha cha mwanafunzi wa kike wa kidato cha sita Sundi George aliyekuwa akisoma katika shule ya sekondari Mwembetogwa.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari  Kamanda wa Polisi Iringa ACP Juma Bwire amesema mnamo Machi 12 mwaka huu akiwa na sare za shule mwanafunzi huyo alitoka nyumbani kwao kuelekea shuleni lakini hakurudi hadi mwili wake ulipopatikana  maeneo hayo.

Kamanda Bwire amesema wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo huku akiwaomba wananchi kutoa taarifa kwa mtu yoyote wanayehi amehusika katika tukio hilo.


from MPEKUZI

Comments