Updates: Mbowe, Katibu Mkuu Wameachiwa....Mnyika na John Heche Wamebakizwa Polisi

Viongozi watatu  wa Chadema walioripoti Kituo Kikuu cha Polisi wakiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji wameachiwa kwa dhamana huku wawili wakitakiwa kubaki.

Viongozi walioachiwa ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu na Dk Mashinji.

Mwalimu amesema Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Serengeti, John Heche wamebaki polisi kwa maelezo kuwa wamekuwa wakikwepa taratibu za dhamana.

Heche na Mnyika hawakuripoti polisi Machi 16, 2018 huku chama hicho kikieleza kuwa moja ya sababu ya wabunge hao kutoripoti ni kutokana na kuhudhuria vikao vya kamati za Bunge mjini Dodoma.

Dk Mashinji ameeleza kuwa viongozi wengine wa chama hicho waliotakiwa kuripoti polisi leo akiwemo mbunge wa Kawe, Halima Mdee wamepata dharura.

“Mdee yupo nje ya nchi kwa matibabu na Ester Matiko yuko Dodoma kwa shughuli za kibunge amechelewa usafiri,” amesema Dk Mashinji.


from MPEKUZI

Comments