Trump ajipanga kuiwekea vikwazo China

Rais wa Marekani, Donald Trump anajipanga kuiwekea vikwazo nchi ya China mara baada ya kugundua kuwa nchi hiyo imekuwa ikiiba utaalam na ubunifu wa biashara za Marekani.

Ikulu ya Marekani imesema kuwa hatua hiyo imefikiwa mara baada ya kufanyika mazungumzo ya muda mrefu bila kufikia muafaka kuhusu jambo hilo.

Aidha, Mpango huo umezua hofu kubwa kuhusu vita vya kibiashara kati ya nchi hizo kwani vikwazo hivyo vitashirikisha ushuru na masharti mengine.

Vilevile huenda Marekani ikawasilisha malalamiko yake kwa Shirika la Biashara Duniani WTO, kulingana na maafisa wa biashara.

Hata hivyo, Bunge la Congress pia linapanga kupitisha sheria ambayo itaipatia serikali uwezo wa kubadilisha mikataba ya biashara za kigeni kutokana na vitisho vya China kununua viwanda vya Marekani.

 Afisa wa biashara nchini Marekani ambaye alizungumza na wanahabari alisema kuwa Marekani ina ushahidi kwamba China inataka kampuni za Marekani kuingia katika ushirikiano na kampuni za China ili kuingia katika soko la taifa hilo kwa lengo la kuzishinikiza kampuni hizo kuhamisha teknolojia yao.

Marekani pia iligundua kwamba China inawekeza katika kampuni muhimu za Marekani na kufanya mashambulio ya mitandao.

Matokeo hayo yanatoka katika uchunguzi ulioagizwa na rais Trump mwezi Agosti kwa jina 301.

Katika kipengee cha 301 cha sheria ya biashara, serikali imejipatia uwezo wa kuwekea vikwazo mataifa ambayo inahisi hayafanyi biashara kwa usawa.

Bwana Trump mara kwa mara amekuwa akilalamika kuhusu ukosefu wa usawa kibiashara kati ya Marekani na China.
Je hatua hiyo inaungwa mkono na wengi?

Kuna wasiwasi mkubwa nchini Marekani kwamba China inatafuta teknolojia ambayo wanaweza kuitumia kijeshi. 


Lakini wanasiasa na viwanda ikiwemo watumiaji wameonyesha wasiwasi kwamba huenda China ikalipiza kisasi.

Bwana Lighthizer amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa China ikalipiza kisasi akidai kwamba Kilimo cha Marekani huenda kikaathiriwa , lakini akasisitiza kwamba hatua hiyo haitaizuia Marekani kuchukua hatua.

Iwapo watalipiza kisasi basi Marekani italazimika kuwalinda wakulima wake.


Pia alisema kuwa anatumai kwamba Marekani itapunguza masharti kuhusu bidhaa za kiteknolojia zinazoingia China.


Credit:BBC


from MPEKUZI

Comments