TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Tatu ( 33 )

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Gafla tukastukia akiichomoa bastola yake na kutonyooshe sisi na Rahma na kwastory nilizo wahi kuzisikia mtaani kweni ni kwamba huyu mzee anatabia ya kutembea na wasichana wadogo japo sikuwahi kumshuhudia na kwa story nyingine nilizo zipata mtaani ni kwamba alimuua mke wake kwa kumpiga rasasi baada ya kufumaniwa akiwa na binti mdogo

ENDELEA
Mlio wa bastola ya mzee Ngoda ukanifanya nifumbe macho huku nikisikilizia ni wapi risasi yake ilipo tu,Swali nililo nalo kichwani kwangu ni kwamba ni wapi risasi ilipo tua kwa maana mwilini mwangu sikusikia maumivu ya aina yoyote na kama imempiga Rahma wangu mbona sijasikia sauti yoyote ya yeye kutoa maumivu.Kwa haraka ni kafumbu macho na kumtazama Rahma na kumkuta akitetemeka kwa woga
“Angalieni nyuma yenu”
Tukageuka na kukuta nyoka mkubwa akining’inia kwenye tawi la mti huku kichwa cheke kikiwa kimetawanywa na risasi aliyo pigwa na Mzee Ngoda

“Mwanajeshi anatakiwa kuwa na hisia za kitu chochote cha Atari kitakacho kuwa karibu yake ila nakushangaa Eddy wewe nyoka yupo nyuma yako wala hustuki kwa kitu cha ina yoyote”
Kutokana na mstuko wala sikujua nimjibu kitu gani mzee ngoda,Rahma akanishika mkono na kunikumbatia huku akiendelea kutetemeka.Mzee Ngoda akapanda kwenye gari na kutuomba na sisi tupande,taratibu nikamshika Rahma mkono na tukapanda kwenye gari na safari ikaendelea ambayo tayari nilisha anza kuitilia mashaka na sikujua ni wapi tunapoelekea.Tukafika kwenye moja ya jumba kubwa lililo jegwa vizuri na Mzee Ngoda akasimamisha gari nje ya jumba hili na akatuomba tushuke kwenye gari

“Karibuni sana wanangu hapa ni nyumbani kwangu”
Mzee Ngoda alizungumza huku akitoa funguo nyingi na kufungua geti la chuma lililopo kwenye jumba hili,kisha akafungua na mlango mwengine na tukaingia ndani japo kuna giza kuba.Akawasha swichi na taa za ndani zikawaka
“Hapa ni kwangu huwa nikiwa na mawazo sana huwa ninakuja huku kupumzika kama wiki kisha ninarudi tena mjini”
“Unakuja kupumzika peke yako?”
“Ndio ninakuja peke yangu na niwatu wengi hawaijui hii nyumba yangu kwa maana ipo porini sana”
“Ni kubwaa”

“Yaa ina eneo kubwa kwa huko nyuma kuna bustani za maua ya kutosha sema sasa hivi ni usiku sana….Hii nyumba niliinunua kwa rafiki yangu alikuwa ni mwanajeshi wa kijerumani kipindi cha miaka ya semanini”
“Ahaa sawa”
Mzee Ngoda akatuonyesha chumba cha kulala ambacho ni kikubwa sana na kina vitu vichache vya dhamani pamoja na kitanda kikubwa cha duara ambacho tangu nizaliwe sikuwahi kulala,nikakichunguza chumba kizima  na kuridhika na mazingira yaliyopo humu ndani.Nikavua nguo zangu na kupanda kitandani na Rahma akafanya kama nilivyo fanya mimi na ikawa ni siku nyingine ya furaha katika mahusiano yetu baada ya kupitia kipindi kigumu cha maisha.Baada ya kupeana haki ianyo stahili kila mmoja akapitiwa na usingizi mzito



from MPEKUZI

Comments