TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Tano ( 35 )

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA  

Taratibu nikafungua pazia la dirisha la sebleni na nusu nipoteze fahamu ila nikajikaza kuendelea kutazama.Kundi kubwa la watu wenye asili ya kijerumani wamewazunguka Rahma na jamaa mmoja wa kizungu huku Rahma akiwa amevalia shela la harusi huku na jamaa suti ya harusi na Rahma ameishika pete yangu aliyo itupa akitaka kumvalisha jamaa kwenye kidole kama nilicho kuwa nimekivaa mimi na nikazidi kuchanganyikiwa baada ya muongozaji wa harusi hiyo akiwa ni Olvia Hitler

ENDELEA
Taratibu nikalifunga pazia na kukaa kwenye kichi huku nikijiuliza ninacho kiona ni kwelia au ni ndoto,Kelele za ngoma zikanifanya niweze kuamini kama ni kweli kwa ujasiri mkubwa nikasimama na kuufungua mlango na kuwafanya watu wate waliopo kwenye eneo nje kunitazama kwa macho makali ambayo si ya kawaida kama ilivyo kwa sisi binadamu.Macho yao yametawaliwa na rangi ambazo si za kawaida kwa haraka haraka ninaweza kuzifananisha na mwanga wa moto wa gesi.

Rahma akabaki akinishangaa kama mtu asiye jitambua aliye kamatwa na bumbuazi kali,Nikaanza kupiga hatua mbili mbele na kuwafanya vijana wawili wa kijerumani kusimama mbele yangu na kunitazama kwa umakini kisha nao wakaanza kunisogela huku taratibu wakianza kubadilika maumbo yao kwa kutoka manyonya kama ya mbwa.Nikaanza kurudi nyuma kwa haraka na nikausukuma mlango ila kwa bahati mbaya nikaukuta mlango ukiwa umejifunga kwa ndani.

Jamaa wakazidi kunifwata na sikuwa na jinsi zaidi ya kaanza kupiga hatua za hakanyaga maua yaliyopo pembezoni mwa ukuta na kuanza kukimbia kuelekea sehemu yenye msitu,Vijana wa kijerumani naa wakanza kunikimbiza na kadri wanavyo kimbia ndivyo  miili yao ikabadilika na kuwa kama mbwa aina ya Bweha(FOX) na kuzidi kunikimbiza.Sikuwa na namna nyingine yoyote zaidi ya kuuparamia mti kwa haraka cha hadi nikakaa juu ya moja ya tawi huku nikihema na jasho jingi lilimwagika.Mwanga wa mbara mwezi ukanisaidia kuwaona jamaa wakiuzunguka mti huku wakinguruma kwa sauti za kutisha sana.Mbwa watu wakaanza kutoa vilioa vya ajabu na kadri mawingu yanavyozidi kuufunika mwezi ndivyo wao wanavyozidi kupata shida katika miili yao na ambayo ikaanza kurudi katika hali kawaida hadi wa kawa binadamu wa kawaida ila hakuna aliye kuwa na nguo miomgoni mwao

Kila kitu ambacho kinaendelea sikuwa ninaamini ni kweli na ninayo jionea,nikajilaza kwenye tawi huku nikiendela kuwatazama jamaa na wakabaki chini ya mti wakiwa wananitazama huku wakinisubiria nishuke.Masaa yakazidi kwenda na kidogo nikaanza kushindana na macho yangu kitika swala zima la usingizi na kila nipojaribu kuyafumbua kwa nguvu zagu zote ndivyo jinsi macho yalivyo zidi kunikatali nakujikuta taratibu nikiyafumba na kausingizi kakanipitia.Nikaanza kuisikia sauti kwa mbali ya Rahma ikiniita na kunilazimu kuyafumbua macho na kukuta mwanga ukiwa umetawala kila sehemu na jamaa sikuwaona,Nikashuka kwenye mti taratibu hadi ninakanyaga ardhi na Rahma akawa amefika kwenye sehemu nilipo
“Eddy ulikuwa wapi?”
Nikamtazama Rahma kwa macho makali yaliyo jaa hasira na sikumjibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kuondoka pasipo kumkibu.Nikapitiliza moja kwa moja hadi sehemu walipo kuwa wakicheza ngoma zao usiku na kuyakuta mazingira yakiwa kama jana mchana tulivyo yaacha na hapakuwa na hata jani linalo onyesha kuwa limekanyagwa.
“Eddy mume wangu si nimekuuliza ulikuwa wapi hujanijibu kitu au hujanisikia?”



from MPEKUZI

Comments