Rais Magufuli Aita Wawekezaji....Adai Tanzania ni Salama na Hakuna Maandamano

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa walitumia njia ya amani ya Tanzania kuwashawishi wawekezaji waje nchini Tanzania na kuwekeza kwa kuwa ni nchi ambayo hana hata maandamano.

Magufuli amesema hayo leo Machi 19, 2018 wakati akizungumza na wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara Ikulu jijini Dar es Salaam.

"Kuna miradi tumeanza ambayo nafikiri inajenga uchumi wa nchi yetu, bomba la mafuta hili ambalo uwekezaji wake ni zaidi ya dolla bilioni tatu itazalisha ajira zaidi ya watu elfu 15 wale wengine ni wengi zaidi kina mama lishe na kadhalika ni nafasi yenu wafanyabiashara na wawekezaji mkatumia hiyo nafasi ili tusiwe wasindikizaji.

" Tukatumia faidi ya nchi yetu kuwa salama na amani na ile ilikuwa pointi kubwa sana kwamba Tanzania wala hakuna matatizo, wala hakuna maandamano wala nini

"Njooni  muwekeze huku na watu wamekuja hiyo kampuni ya Total inajenga bomba ambalo linapita kwenye wilaya zaidi ya 84 ile ni faidi kubwa kwa watu wanaolewa hiyo ni nafasi kubwa" alisema Magufuli


from MPEKUZI

Comments