Paul Makonda Awaomba Msamaha Wananchi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mh. Paul Makonda amefunguka na kuwaomba msamaha baadhi ya wananchi ambao ameshindwa kutimiza ndoto zake na kusema anaamini ataendelea kuwatumikia na kujitahidi kuweza kugusa maisha ya kila mmoja.

Paul Makonda amesema hayo siku mbili baada ya kutimiza miaka miwili toka ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kusema kuwa ndani ya miaka miwili akiwepo madarakani anaamini amegusa maisha ya watu kwa kutumia kipaji chake, uwezo wake wote.

"Asante Mungu kwa neema zako, kama usingekuwa upande wangu na Dunia iseme sasa. Nawashukuru sana sana watumishi wenzangu Kwa kunivumilia na kunielewa katika kutimiza majukumu yangu. Zaidi nawashukuru sana wananchi naimani nimejitahidi kuwatumikia Kwa moyo wangu wote na vipaji vyote na pale niliposhindwa kutimiza ndoto yenu mnisamee"

Makonda aliendelea kufafanua na kutoa ahadi yake kwa wananchi kuwa

"Zaidi nawaahidi nitaendelea kujituma zaidi ili niyaguse maisha ya kila mmoja wetu kama ambavyo Serikali ya awamu ya 5 inavyokusudia. Mwisho si kwa umuhimu ni Kwa wadau wa maendeleo naomba mfahamu kila cent mliyoitowa ina thamani kwangu na kwa wananchi wangu. Tumefanya Mambo mengi na hakika na tumegusa na hata kuleta faraja Katika maisha ya Watu wengi. Kwakutambua mchango wenu ninaandaa siku ya kuwatambua na kuwatunuku tuzo kama asante yangu kwenu"

Machi 13,  2016 Paul Makonda aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam


from MPEKUZI

Comments