Mwigulu Nchemba Awachana Wanafunzi Na Harakati Zao Za Siasa

Waziri wa Mambo ya ndani, Dk Mwigulu Nchemba amewataka wanafunzi kuachana na harakati za kutengeneza  taswira mbaya za serikali  badala yake kuwa na mitazamo chanya.

Aliyasema hayo jana katika kongamano la UNILIFE lililofanyika Chuo cha Biashara (CBE), ambalo liliandaliwa na Mbunge wa Viti maalum, Ester Mmasi.

Alisema wanafunzi hawatakiwi kufanya harakati ili wawe adui wa serikali kwani yenyewe haina muda wa kushughulikia mashinikizo ya wanafunzi.

“Nilishawahi kufanya harakati nikiwa chuoni na nilipewa jina la Chifu..majina yangu yamekuja kujulikana nikiwa serikalini lakini nilikuwa napinga baadhi ya ajenda za Taifa ambazo niliona hazina manufaa,” alisema Dk Mwigulu.

Alisisitiza kuwa wanafunzi wengi kwa sasa wamekuwa wakiitafuta taswira mbaya ya serikali bila  kuangalia masuala mengine yanayopaswa kuungwa mkono.

“Kuwa kijana mwema chuoni sio kwa kuwa kimya Bali kuwa na mitazamo chanya naukiona mwanazuoni anabisha jambo jema ujue kuna kasoro,” alisema


from MPEKUZI

Comments