Zitto Kabwe amemtembelea Samatta Ubelgiji

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe leo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii amewajulisha watanzania kuwa amefanikiwa kufika nyumbani kwa nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta.

Zitto amefika nyumbani kwa Samatta nchini Ubelgiji katika mji wa Genk na kumjulia hali na amethibitisha kuwa Samatta anaendelea vizuri.

==>Huu ni ujumbe wa Zitto Kabwe
Jana jioni nilikwenda Genk, hapa Ubelgiji, nyumbani kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ndugu Mbwana Ally Samatta, ambaye ni mchezaji wa Klabu ya KRC GENK inayoshiriki Ligi Kuu ya hapa Ubelgiji.

Nimefurahi kupita kumsalimu na kumjua hali Samatta, nimefurahi zaidi kumkuta akiwa ni mzima wa afya na anashiriki mazoezi ya timu yake bila shida. Inatia moyo zaidi kuona Kijana huyu mwenzetu wa Kitanzania namna anavyofanya kazi kwa bidii ili aweze kufanikiwa zaidi. Namuomba Mola amuwezeshe kutimiza ndoto zake.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Genk
Ubelgiji
Februari 13, 2018


from MPEKUZI

Comments