Rais Magufuli Aomboleza Kifo cha Mwanafunzi wa NIT Aliyepigwa Risasi na Polisi

Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametuma salamu za pole kwa familia ya Akwilina Akwilini aliyeuawa baada ya kupigwa na risasi katika maandamano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Februari 16, 2017 eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam

Katika salamu hizo, Rais Dkt Magufuli amesema kwamba amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo hicho na hivyo ameviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo.

“Nimesikitishwa sana na kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji (NIT). Natoa pole kwa familia,ndugu,wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huu. Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili.”

Akwilina alikumbwa na umauti wakati Polisi walipokuwa wakitawanya maandamano ya CHADEMA walipotaka kwenda kwenye Ofisi za Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni kuhoji kwanini mawakala wao hawajaaapishwa.



from MPEKUZI

Comments