Mambosasa atoa onyo kali kwa walioachiwa kwa Msamaha wa Rais

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Jijini Dar es salaam Lazaro Mambosasa, amesema wahalifu waliotoka jela kwa msamaha wa Rais hawatasita kuwarudisha tena jela iwapo wataendelea na tabia za uhalifu.

Kamanda Mambosasa ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na waandihsi wa habari alipokuwa akiwapa taarifa za uhalifu, na kusema kwamba watu wanaoongoza kwa vitendo vya uhalifu ni wale waliotoka kwa msamaha wa Rais, na kwamba wanatumwa na wenzao walio jela.

Akiendelea kuzungumzia suala hilo Kamanda Mambosasa amesema watu hao wamekuwa wakirudia maeneo walioficha silaha kabla hawajakamata na kufungwa, na kuzichukua kuzitumia kwenye matukio ya uhalifu, huku wakendelea kuwasiliana na wale ambao bado wako gerezani kujua wameweka wapi silaha ili kuzitumia kwenye kazi zao, na kisha kuwapelekea posho.

“Taarifa tulizonazo baada ya wahalifu wengine waliochiwa kwa msamaha wa Rais, wachache hawataki kubadili tabia zao, wanakwenda kufichua silaha ambazo walilizika ardhini na sasa wanazifukua kwa ajili ya kuanza kuzitumia. Ninatoa onyo kwa mtu yeyote ambaye amepata msamaha, badala ya kumshukuru Mungu akabadili tabia akaanza kuishi kwa kufuata sheria za nchi, anaenda kufukua silaha mahali alipoficha kwa ajili ya kuendeleza vitendo vya uhalifu, niwaambie hawatabaki salama, tutawarudisha huko walikotoka”, amesema Mambosasa.

Kufuatia tukio hilo Kamanda Mambosasa amewataka watu waliopewa msamaha na Rais na kuwa huru, uacha kabisa matendo maovu, na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano pale wanapohisi kuna mtu anafanya vitendo vya uhalifu.


from MPEKUZI

Comments