Wananchi Mkoani Kagera Watakiwa Kufuatilia Na Kuhoji Kuhusu Miradi Ya Kimaendeleo Katika Kata Zao.

Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera.
Wananchi katika kata ya Katoma Mkoani Kagera wametakiwa kufuatilia kwa kina na kuhoji viongozi wao kuhusu miradi mbalimbali ya kimaendelao inayotekelezwa katika kata hiyo.
 
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Kiserikali  la Faraja For Hope And Development (FAHODE) bwana Antidius  Augustine wakati akiongea  na wananchi wa kata ya Katoma katika mkutano wa hadhara na kuwataka wananchi hao kuweza kufuatilia kwa kina miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika kata hiyo ikiwemo sekta ya maji na kuibua changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
 
Shirika hilo lisilo la kiserikali linajiusisha na ufatiliaji wa uwajibikaji wa jamii katika sekta ya majii kwa kata sita za halmashauri ya Bukoba zikiwa ni pamoja na Kemondo, Katoro,Katerelo,Maruku, Katoma na Ibwela.
 
Bwana Antidius amesema kuwa shirika hilo litaendelea kuijengea jamii elimu kuhusu masuara mtambuka  ili kutumia vizuri rasilimali zilizopo na kupanua wigo wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuendelea kutumia maji safi na salama kila siku.
 
Amewataka wananchi kukaa karibu na viongozi wao ili kuhakikisha miradi ya kimaendeleo haikwami kwani kwa kufanya hivo kutawawezesha pia kujua changamoto zinzokwamisha miradi hiyo na kuongeza kuwa FAHODE imekuwa chachu ya miradi mingi kukamilika  kwa wakatina kuwafikia walengwa kutokana na ushirikiano ambao wanazidi kupewa na wananchi hao.
 
Kwa upande wake diwani wa kata ya Katoma mh Deusdelith Rwekaza amesema kuwa wananchi wa kata hiyo pamoja na kata nyingine ambapo shirika hilo linahudumu kutumia vizuri elimu inayotolewa ili iweze kuwanufaisha katika maisha ya kila siku.
 
Aidha mh Rwekaza emewataka wananchi wa kata hiyo kuwa na utamaduni wa mara kwa mara wa kusafisha vyanzo mbalimbali  vya maji vinavyopatikana katika kata hiyo ikiwemo chemichemi  na vyanzo vingine.


from MPEKUZI

Comments