Tanzania kujumuishwa kati ya nchi 7 zitakazowekewa vikwazo na Marekani

Serikali ya Marekani ina mpango wa kuziongeza Nchi nyingine 7 ikiwemo Tanzania kwenye orodha ya Nchi ambazo Raia wake wamewekewa zuio/vikwazo vya kuingia Nchini humo ambapo Nchi nyingine kwenye hizo 7 ni Nigeria, Sudan, Eritrea, Myanmar, Belarus na Kyrgyzstan.

Vyombo vya habari Marekani vimeripoti kuwa baadhi ya Nchi VISA zinaweza zisifungiwe kabisa bali zitakua ngumu kupatikana kwa masharti (za biashara na matembezi) Maafisa wamesema bado orodha haijakamilika kwani mpaka J'nne Ikulu ilikua inajadili kuongeza Nchi nyingine 1 au 2.

Ripoti hiyo imesema baadhi ya Nchi hizi 7 Raia wake wameongoza kwa kupitiliza muda wa kukaa Marekani kulingana na VISA walizopewa, kwa mwaka 2018 pekee 24% ya Raia wa Eritrea walipitiliza siku za kukaa Marekani, Raia wa Nigeria kwa asilimia 15, Sudan 12%. 

Leo Jumatano Januari 22, 2020 kaimu balozi wa Marekani, Dk Inmi Patterson akihojiwa na Redio Clouds amethibitisha suala hilo baada ya jana jioni taarifa za Tanzania na nchi hizo kuwekewa vikwazo kuanza kusambaa katika mitandao ya kijamii. 

Soma zaidi :https://www.nytimes.com/2020/01/21/us/politics/trump-travel-ban.html


from MPEKUZI

Comments