Serikali Yaandaa Mkakati Wa Miaka Mitano Wa Kukuza Zao La Pamba

Serikali imesema imetengeneza mkakati wa miaka mitano kuhusu sekta ndogo ya pamba ili kukidhi mahitaji ya soko na upatikanaji wa pembejeo kwa wakulima nchini.

Kauli hiyo Imetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe wakati akifungua mkutano wa kamati ndogo ya wadau wa kilimo iliyokutana jijini Dodoma.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Wakuu wa mikoa inayolima zao la pamba nchini ambao wamepokea na kujadili taarifa ya kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza changamoto zinazoikabili tasnia na kutoa mapendekezo ya utatuzi wake.

Kamati ndogo ya wadau iliundwa Octoba mwaka jana jijini Mwanza kwa lengo la kuja na mapendekezo ya utatuzi wa changamoto za zao hilo nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mh Bashe amesema kikao hicho ni uhimu ili kutengeneza mustakabali mzuri wa tasnia ya pamba kwenye mikoa 17 inayolima zao hilo.

Bashe amesema msimu ujao wa kilimo cha pamba unapaswa uwe mzuri na usiwe na matatizo licha ya mikoa michache bado ina takribani asilimia 20 ya pamba isiyonunuliwa hadi sasa.


from MPEKUZI

Comments