PICHA: Ujenzi Wa Barabara Za Juu Makutano Ya Ubungo (Ubungo Interchange)

Maendeleo ya Ujenzi wa Barabara za Juu katika Makutano ya Ubungo (Ubungo Interchange). Mradi huo wa Ujenzi katika Makutano  ya Barabara za Mandela, Morogoro na Sam Nujoma (Ubungo Interchange) unaendelea kwa kasi kubwa na umefikia asilimia 65 kwa mradi mzima na sehemu ya gorofa ya pili ambayo itapitisha magari yanayotumia barabara ya Morogoro imefikia asilimia 75.

Mradi huo unatarajiwa kuondoa adha ya msongamano mkubwa katika makutano ya barabara hizo pindi utakapokamilika. PICHA NA IKULU


from MPEKUZI

Comments