Mamia ya Wananchi wa IRAQ Waandamana Kulitaka Jeshi la Marekani Liondoke Nchini Mwao

Mamia ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad, wakidai vikosi vya Marekani viondoke Iraq.

Kiongozi mwenye ushawishi wa dhehebu la Shia Iraqi, Moqtada al-Sadr awali alitoa wito kwa mamilioni ya raia kushiriki maandamano ya Ijumaa, karibu na ubalozi wa Marekani nchini Iraq.

Vikosi vinavyoungwa mkono na Iran ni miongoni mwa wanaondamana.

Hatua ya Marekani ya kumuua kamanda wa kijeshi wa Iran, Jenerali Qasem Soleimani, Januari 3 katika uwanja wa Baghdad uliongeza uhasama

Pia aliyeshambuliwa kwa ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani ni Abu Mahdi al-Muhandis, mmoja wa makamanda wa Iraq ambaye kundi lake la Kataib Hezbollah linaloungwa mkono na Iran pia aliuawa katika shambulio hilo.

Iran ilijibu shambulizi la mauaji ya Jenerali Soleimani kwa kutekeleza shambulizi la kombora dhidi ya kambi mbili za kijeshi za Marekani nchini Iraq.


from MPEKUZI

Comments