Kingwalla: "Walipanga Kuniangamiza na Walitaka Nitumbuliwe Uwaziri"

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamis Kigwangalla, ameeleza kuwa kwa sasa anaishi kwa hofu na tahadhali kubwa juu ya uhai wake kutokana na kuwepo kwa kundi la watu wanaomuwinda wakitaka kumuangamiza huku wengine wakimfanyia mipango ya kumuharibia ili atumbuliwe uwaziri.

Kupitia akaunti yake ya instagram Kigwangala ameweka wazi kuwa hata alivyopata ajali aliwekewa ulinzi mkali wodini ili wabaya wake wasiweze kummalizia kwa namna yoyote.

Kupitia instagram yake ameandika hivi; Sikusudii kufanya press conference. Watu wengi wamenishauri niishie hapa. 

Team yangu imefanya kazi nzuri, imenipa uthibitisho wa majina ya wanaotaka nichafuliwe ili niondolewe uwaziri. 

Bahati mbaya hakuna cha kunichafua nacho, wanapika hadithi za kitoto na kurudia tu. Walidhani ningekaidi maelekezo ya Mhe. Rais juu ya mgogoro wa ndani ya Wizara yetu ili Rais achukie aniondoe, wakakwama. Sikukaidi. 

Wakaona wafanye mwendelezo kupitia gazeti, sijataka kujibishana nalo, tutakutana mahakamani ambapo mbivu na mbichi zitajulikana, ukweli utawekwa wazi na rekodi itakaa sawa. Sijashangaa kuwa wahusika ni wale wale wa kipindi kilichopita.

Hakuna jipya. Sababu ni deal yao binafsi, ambayo haitekelezeki bila ridhaa ya Waziri, na bahati mbaya kwao Waziri ni mimi; walitamani nisiwepo watafune pesa za serikali vizuri, wamekwama. 

Tutaendelea kudhibiti kimya kimya. Kwa wanaokumbuka wakati nimelazwa ICU na baadaye wodini, ilikuwa ngumu sana kunitembelea na kuniona. 

Paliwekwa ulinzi mkali sana na watu wote walizuiliwa kuingia isipokuwa kwa kibali cha Ikulu, hadi Mawaziri wenzangu hawakuruhusiwa. 

Nilishangaa sana lakini niliambiwa ndiyo hivyo. Baadaye nikaja kujua kuwa kuna watu walipanga njama za kuniua na hiyo ingeweza kuwa fursa kwao kunimalizia. 

Baada ya kuteuliwa tu Wizara hii kulizuka mtafaruku mkubwa sana juu ya usalama wangu, nilifuatiliwa kila kona mpaka serikali ikanipa walinzi, nilibisha kwa kuwa sipendi attention sana lakini nililazimishwa na kuambiwa nipo kwenye ‘threat’! Sikuwa na option. 

Nilianza kuishi kwa hofu na mashaka sana. Hivyo, baada ya ajali na yaliyotokea kutokea nililazimika kuwa makini zaidi. Imani yangu kwa kila mtu ilipungua. Nikawa ‘alert’ wakati wote. 

November 2019 nililetewa taarifa za kutisha, nikaongeza umakini. Team yangu imenisihi nisiweke majina hadharani na kwamba wanawafuatilia wahusika kwa ukaribu na watazijulisha mamlaka kwa hatua stahiki zaidi. Watu wa karibu sana na mimi nimewapa mpango na taarifa zote na wanajua cha kufanya endapo chochote kitanitokea. Kuna mbinu nyingi za mapambano. Tuendelee tu!


from MPEKUZI

Comments