Jeshi la Polisi Lapangua Tuhuma za Mkuu wa Wilaya....."Wamiliki wa mabasi waliotajwa na DC Sabaya hawajahujumu miundombinu ya reli "

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limesema hakuna hujuma wala uharibufu wa miundombinu ya Reli katika eneo la Kijiji cha Rundugai Wilayani Hai kama zilivyoelezwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Lengai Ole Sabaya .

January 19 mwaka huu Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya akiwa katika Kijiji cha Rundugai akikagua ukarabati wa Reli alitoa agizo la kukamatwa kwa wafanyabiashara wawili wa mabasi kwa tuhuma za kuunda genge la uharifu ili kuathiri usafiri wa treni ya abiria kati ya Dar,Moshi hadi Arusha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Salum Hamdun, amesema kuwa baada ya DC kutoa tuhuma hizo na kuagiza wafanyabiashara wawili wa Mabasi ya Abiria, kujisalimisha polisi, walitii agizo hilo na baada ya kutoa maelezo walitoka kwa dhamana.

"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa hakuna miundombinu ya Reli iliyoharibiwa au kuhujumiwa katika himaya hii kwa maana ya kipande cha kutoka Moshi kuelekea Arusha, ambapo mpaka sasa kimeshakarabatiwa kwa Kilomita 23 na kazi inaendelea" amesema RPC Kilimanjaro.


from MPEKUZI

Comments