Ajira Mpya Kada ya Afya Zilizotangazwa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Taasisi ya Benjamin William Mkapa inatekeleza Mradi wa Kuimarisha Mifumo Stahimilivu na Endelevu ya Afya (RSSH) kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund).
 
Mradi huu una lengo la kuimarisha huduma za afya ngazi za vituo katika Mikoa kumi (10) iliyopewa kipaumbele na mradi huu ambayo ni Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Geita, Kagera, Katavi, Tabora, Dodoma na Kigoma.
 
Hivyo, Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamin William Mkapa inapenda kuwatangazia wahitimu wa kada za afya nchini kuwasilisha maombi ya nafasi za kazi, kuanzia tarehe 20/01/2020 ili kujaza nafasi mbalimbali za Kada ya Afya katika Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati.
 
Nafasi zinazotangazwa ni zifuatazo:-
1. Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II
Waombaji wawe na Stashahada (Diploma) ya Uuguzi ya muda usiopungua miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.
 
2. Muuguzi Daraja la II
Waombaji wawe na Cheti cha Uuguzi cha miaka miwili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa (Enrolled) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.
 
3. Tabibu Daraja la II
Waombaji wawe na Stashahada (Diploma) ya Utabibu ya muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
 
4. Tabibu Msaidizi
Waombaji wawe wamehitimu Astashahada (Cheti) ya miaka miwili ya Tabibu Wasaidizi (Clinical Assistants Certificate) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
 
5. Mteknolojia Daraja la II (Maabara)
Waombaji wawe na Stashahada (Diploma) ya Sayansi ya Maabara ya muda wa miaka mitatu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa na Mabaraza ya Taaluma.
 
6. Mteknolojia Msaidizi (Maabara)
Waombaji wawe wamehitimu Astashahada (Cheti) ya miaka miwili katika fani ya Maabara kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Mabaraza yao pale inapohusika.

==>> Kutuma Maombi <<BOFYA HAPA>>


from MPEKUZI

Comments