CUF Nao Wajitoa Uchaguzi Serikali za Mitaa.....Waitaka Serikali Kutotumia Nembo Yake

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba amesema Chama chake hakitoshiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na hakiutambui uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Mwezi huu mwishoni kwa madai ya ukiukwaji wa Haki na Sheria katika mchakato wake

Profesa Lipumba ametoa msimamo huo  leo Jumanne Novemba 12, 2019  wakati akitoa maazimio ya kikao cha baraza kuu la uongozi la CUF.

CUF kinakuwa chama cha siasa cha sita kujitoa katika uchaguzi huo baada ya Chadema, ACT-Wazalendo, NCCR-Mageuzi, UPDP na Chauma.

Katika maelezo yake Profesa Lipumba amesema  baraza hilo limetafakari kwa kina na kuona hakuna umuhimu kushiriki uchaguzi baada ya hoja zao tatu walizoziwasilisha serikalini kutofanyiwa kazi.

Profesa Lipumba amewataka asilimia nne ya wagombea wa chama hicho waliopitishwa kugombea kujitoa na kuiomba Tamisemi kutotumia nembo ya chama hicho kwenye uchaguzi huo.


from MPEKUZI

Comments