Baraza la wazee la Chadema Labariki Chama Hicho Kujitoa Uchaguzi Serikali za Mitaa

Baraza la wazee la  Chadema limebariki uamuzi wa chama hicho kujitoa kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Novemba 8, 2019 mwenyekiti wa baraza hilo, Hashim Juma Issa amesema ilikuwa lazima chama hicho kijitoe kutokana na kutengenezewa mazingira ya kufanya hivyo.

Issa amekwenda mbali zaidi na kuwataka wanachama wao kote nchini kutotoa ushirikiano kwa viongozi watakaoteuliwa kushika nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo.

“Hatuna sababu ya kushirikiana nao kwa kuwa wameteuliwa na sisi tunahitaji viongozi wa kuchaguliwa na wananchi kidemokrasia,” amesema.


from MPEKUZI

Comments