ACT-Wazalendo Nao Watangaza Kujitoa Uchaguzi Serikali za Mitaa

Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe, ametangaza kuwa chama hicho hakitoweza kushiriki tena Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kwa kile alichokieleza kuwa wagombea wao zaidi la Laki 160, wameenguliwa na kubaki na wagombea Elfu 6 pekee, sawa na asilimia 4 ya wagombea wote.

 Tamko hilo amelitoa leo Novemba 8, 2019, baada ya Kamati ya Uongozi wa Chama hicho na  kuagiza ile asilimia 4 ya wagombea wote waliopitishwa, wajiengue kushiriki katika uchaguzi huo kwa kuwa haki haijaweza kutendeka.

"Sisi hatutashiriki kwa sababu tumeondolewa, toka juzi tumekuwa na mashauriano na vyama vya siasa nchini, wenzetu wametoa maamuzi yao jana, sisi tumetoa maamuzi yetu leo, tutawajulisha wananchi hatua gani tutaenda kuchukua kwa ajili ya kulinda kilicho chetu, wao wametuondoa asilimia 96 na sisi tumewasaidia kuiondoa ile asilimia 4 ili tusishiriki kabisa" amesema Zitto.

Jana Novemba 7, 2019, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilitangaza rasmi kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, siku ya Novemba 24, ambapo pia kiliwataka wagombea wake walioenguliwa kutokata rufaa.


from MPEKUZI

Comments