Wasiooa na kuolewa kucharazwa bakora Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema kuwa hivi sasa wanatumia bakora katika kila jambo hata kwa watu ambao wanakaa tu nyumbani wakati wamefikisha umri wa kuoa na kuolewa.

Chalamila amesema kuwa bakora ndiyo njia pekee ambayo inasaidia katika kunyoosha mambo.

"Maana siku hizi tumeanza kutumia viboko kwenye kila jambo hata tukikuta umekaa pale nyumbani uolewi ni bakora tu kwamba nenda katafute mume, tunakuona umekaa pale nyumbani huoi ni bakora tu wewe nenda katafute mke.," amesema Chalamila na kuongeza kuwa

"Kuna umri ambao unatosha lazima uchangamshwe kwa hiyo viboko vinasaidia," amesema 

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa huo, alitawala kwenye vyombo mbalimbali vya habari baada ya kuonekana anawachapa bakora baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kiwanja, iliyopo Chunya mkoani Mbeya, baada ya kuteketeza kwa moto mabweni yao.


from MPEKUZI

Comments