Nchi Wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu Zajadili Halia ya Amani, Usalama

Na Mwandishi wetu, Brazzaville
Nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu wakutana jijini Brazzaville na kujadili hali ya amani na usalama katika maeneo yaliyokubwa na ugonjwa wa ebola.

Wanachama hao walikutana na pamoja na wataalamu wa afya kutoka nchi hizo kuanzia tarehe 11 hadi 14 Oktoba 2019, jijini Brazzaville Jamhuri ya Kongo

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianao wa Jamhuri ya Kongo, Mhe. Jean Claude Gakosso ambapo alisema kuwa mkutano huo uliitishwa kwa ajili ya kujadili masuala makuu mawili ikiwemo hali ya ugonjwa wa ebola katika ukanda wa maziwa makuu pamoja na hali ya usalama katika maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa wa ebola.

Kuhusu hali ya ugonjwa wa ebola, ilielezwa kwamba nchi ya DRC ndiyo iliyoathirika zaidi na ugonjwa huo. Ikielezwa kwamba zaidi ya watu 3000 wameathirka na ugonjwa huo na kati yao zaidi ya 2000 wamepoteza maisha ambapo maeneo yaliyoathika zaidi ni yale ya mashariki mwa DRC ambayo ni Kivu Kaskazini, Ituri na Kivu Kusini.

“Juhudi mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ya DRC hadi sasa kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na wadau wengine katika kupambana na ugonjwa huo ni kutoa chanjo ya kinga ya ugonjwa huo na elimu kwa wananchi wa maeneo yaliyoathirika na ugionjwa huo” alisema Waziri Gakosso

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya kutoka ukanda wa maziwa makuu, imeelezwa kuwa hali ya maambukizi kwa sasa imepungua katika maeneo hayo.

Aidha, pamoja na jitihada hizo za serikali ya DRC kwa kushirikiana na wadau wengine katika mapambano hayo kumekuwa na changamoto ya usalama kutokana na kuendelea kuwepo kwa makundi ya waasi katika maeneo hayo ambayo yamekwamisha jitihada hizo

Katika hatua nyingine, mkutano wa waratibu wa kitaifa kutoka nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu kutoka nchi zote 12 walikutana na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo, michango ya wanachama,  suala la ajira, hali ya ulinzi na usalama katika nchi wanachama wa pamoja na suala la watu wasio na utaifa

Mikutano hiyo miwili imetangulia mkutano mkuu wa mawaziri wa mambo ya Nje kutoka nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu utakao fanyika leo, Brazzaville ambapo ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro

Nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu ni pamoja na Angola, Burundi, Jamhuri ya Kati, Demokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo, Kenya, Rwanda, Sudan, Sudani Kusini, Tanzania, Uganda na Zambia.


from MPEKUZI

Comments